Mwanariadha maarufu AFARIKI baada ya kuhusika katika ajali barabarani
- Raia wa Uingereza mwenye asili ya Jamaica na mchezaji wa kuruka viunzi Germaine Mason alifariki baada ya kuhusika katika ajali mbaya
- Ajali hiyo ilihusisha pikipiki alipokuwa akiendesha akishindana na mwanariadha mwenye mbio zaidi ulimwenguni Usain Bolt
Raia wa Uingereza mwenye asili ya Jamaica Germaine Mason aliaga dunia baada ya kuhusika katika ajali mbaya sana ya barabarani Alhamisi Aprili 20.
Germaine alikuwa akiendesha pikipiki alipohusika katika ajali hiyo. Germaine, ambaye ni rafiki wa karibu wa Usain Bolt alipoteza maisha alipokuwa akiandamana na marafiki baada ya kutoka hafla Kingston, Jamaica.

Habari Nyingine: Wanasiasa 6 wa kike wanaoaminika kuwa WAREMBO zaidi nchini (picha)
Ripoti zilizofikia TUKO.co.ke zinaonyesha kuwa mchezaji huyo wa miaka 34 ambaye alishinda fedha wakati wa mashindano ya Olimpiki Beijing 2008 alikosa kudhibiti pikipiki yake alipokuwa akijaribu kukwepa gari lililokuwa likimjia kutoka mbele.
Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE!
Alikuwa ametoka sherehe na marafiki wake akiwemo Usain Bolt ambaye ni mshindi mara tatu katika michezo ya Olimpiki na mwanariadha mwingine Michael Frater.
Habari Nyingine: Shirika hili la Marekani ladaiwa KUMFADHILI Raila Odinga
Mason alipenda sana pikipiki zake na alionekana kuziendesha katika mataifa aliyozuru. Baada ya kuaga dunia, watu wengi maarufu ulimwenguni walituma jumbe za rambirambi.
Subscribe to watch new videosSubscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: aron.mtunji@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaIR4f5JmpLCZnpa%2Fqq3DoZhmpZGWv7ay1GaYn5minriqecGamJ2ZXa6ubrfUoaysoZuWeqyt06KimmWRn66ttYybmKuZkpa%2ForrIZ5%2BtpZw%3D