Raila Odinga na vinara wa muungano wa NASA wapinga matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa na IEBC
- Raila Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi ambayo yanapeperushwa kwa sasa kwenye runinga za kitaifa
- Raila anadai kuwa tume ya IEBC inatangaza matokeo hayo bila fomu ya 34A kama inavyotakikana na sheria
Mgombea wa urais wa muungano wa NASA,Raila Odinga amepinga matokeo yanayotangazwa na tume ya IEBC hivi sasa.
Habari Nyingine: Picha ya Diamond platinumz akiwa mchanga itakuacha kinywa wazi

Habari Nyingine: Uhuru na Raila ni wapenzi wa aina gani? Binti Mkenya awalinganisha
Raila alidai kuwa tume hiyo haina fomu ya 34A ambayo huwa na matokeo ya urais na ambayo hutoka katika vituo vya kupigia kura ikiwa imewekwa sahihi na maajenti wa vyama vya kisiasa.
Malalamishi hayo yaliungwa mkono na viongozi wengine akiwemo James Orengo na Musalia Mudavadi waliodai kuwa IEBC ilikuwa ikitangaza matokeo hayo kinyume na sheria bila fomu hiyo.

Habari Nyingine:Wanawe Seneta Boni Khalwale wahusika katika ajali ya barabarani
Akizungumza na vyombo vya habari, Jumatano Agosti 9 usiku, Raila alisema kuwa walikuwa wameafikiana na tume ya IEBC kwamba fomu hiyo ingewasilishwa kabla ya matokeo kuanza kutangazwa.
Lakini Raila alishangazwa ni vipi matokeo yalikuwa yanaendelea kutangazwa ilhali hawajapokea fomu hiyo.
Raila alisisitiza kwamba IEBC imekiuka sheria na kuvuja kitengo cha 39 cha katiba ya Kenya.

“ Matoke yanayotolewa na IEBC sio ya kweli, tunayspings vikali na tunataka tume hiyo kutangaza matokeo ya ukweli,”Raila alisema
Aidha,NASA ilidakuwa ilikuwa inaongoza katika vituo 377 vya kupigia kura.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaYV6f5BmqZqhnJZ6sLDIp56aZZ6Were1zZqpmmWnlnquwdSnnpqmn2LEonnNmqqaZaeWvaq6xppkppmkpLimu4yymGatk52uqMHZomSymZ6Wxm%2B006aj